Tafadhali Subiri .....
Kuhusu NAIC

Kwa sasa Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji(NAIC) ndiyo taasisi pekee inayotoa na kudumisha huduma ya Kituo cha Uhimilishaji nchini Tanzania. Kituo hicho kina vifaa vyote na wataalamu wa kiufundi kufanikisha zana hii muhimu kwa uzalishaji wa mifugo nchini. Hivi ni pamoja na maabara ya uchakataji wa mbegu za madume, mtambo wa kuzalisha kimiminika cha hewa baridi ya naitrojeni, madume na mashamba ya malisho, ofisi, karakana, nyumba za wafanyakazi, na vifaa vya kilimo.

Dira na Dhamira

Kuboresha uzalishaji wa mifugo kwa kutumia mbegu bora za madume ili kukuza kipato na kutokomeza umaskini kwa mfugaji

Kutafuta madume bora kokote duniani ya kuzalisha mbegu bora na kuzisambaza kupitia wahimilishaji kulingana na mahitaji ya wafugaji kwa lengo la kuborsha koo-safu za mifugo yao ili kuongeza uzalishaji wa nyama na maziwa nchini

Malengo

Lengo la kuanzisha kuanzisha kituo cha NAIC mwaka 1974/75 ilikua ni:-

1. Kuzalisha ng'ombe chotara kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa na nyama ili kuboresha maisha.

2. Kupunguza matumizi ya kununua wanyama hai, maziwa, na bidhaa za maziwa kutoka nje na hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumiwa katika uagizaji huo.

3. Kutoa kwa wafugaji wadogo wanyama wenye uwezo wa kuzalisha kwa bei nzuri, hivyo kumpatia chanzo cha kipato kupitia mauzo ya maziwa kutoka kwa wanyama wa mseto / wenye ubora wa juu.

4. Kudhibiti magonjwa ya vizazi  (kama vile Ugonjwa wa kutupa mimba  (Brucellosis) n.k.) kwa wanyama  yanayosambazwa na Ng’ombe wakati wa kupanda.

Historia

Uanzishwaji wa Kituo cha Uhimilishaji nchini Tanzania ulianza mwaka 1958 na 1959 wakati baadhi ya wafugaji wenye mifugo katika maeneo ya Arusha na Kilimanjaro walileta mbegu za madume zenye joto la kawaida kutoka Kabete, Kenya. Kituo cha Utafiti wa Mifugo kilichoko Magharibi mwa Kilimanjaro na Kituo cha Uzalishaji wa Mifugo huko Mpwapwa pia vilipata mbegu za madume kutoka Kabete kipindi hicho hicho kwa madhumuni ya majaribio ya uzalishaji.

 

Kipindi cha mwaka 1961 hadi 1963, wafugaji wadogo katika maeneo ya Kilimanjaro na Arusha walionyesha shauku ya huduma ya  Uhimilishaji na kuanzisha Vikundi vya Ng’ombe wa Maziwa ambavyo walilipa ada ambazo zilinunua mbegu za madume na vifaa kwa ajili ya matumizi katika huduma hii, huku Serikali ikitoa usafiri na wataalamu wa kiufundi. Kipindi hicho hicho Kituo cha Utafiti wa Mifugo Magharibi mwa Kilimanjaro kilikusanya mbegu za madume kutoka kwa ng'ombe wa Jersey kadhaa kwa ajili ya matumizi katika kundi lao pamoja na wafugaji wadogo walioko jirani.

Mwaka 1968 Serikali ilifanya huduma ya Uhimilishaji iwe ya bure kwa kila mtu. Vikundi vya mifugo vilivyotoza mbegu tatu kwa jumla ya Tsh. 12.50  viliacha kufanya kazi na kufa.

Mwaka 1966/67 Serikali ilianzisha kituo cha mifugo huko Mpwapwa kwa ajili ya ukusanyaji wa mbegu za madume. Kituo hicho awali kilizalisha mbegu za madume zilizohifadhiwa katika maziwa ya nazi, na takribani mwaka 1968 kilitoa utaratibu wa kuhifadhi kwa kutumia kimiminika cha hewa baridi ya naitrojeni kwanza kwa kutumia "ampoule" na mirija ya Kifaransa.

Baada ya kufunguliwa kwa kituo cha ng'ombe cha Mpwapwa, mbegu za madume zilipatikana zaidi na huduma ya Uhimilishaji ilienea katika mikoa mingine kama vile Tanga, Mwanza, Dodoma, Mtwara, Mbeya, Iringa, Morogoro, Pwani, na Mara. Mwaka 1972 mradi uliandikwa ili kuanzisha Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji(NAIC) huko Usa River, Arusha. Kituo hiki kilianzishwa kwa msaada wa Sweden.

 

Mwaka 1974 Serikali ya Cuba ilikubali kujenga kituo cha ng'ombe kwa ajili ya madume Tanzania huko Butiama. Kwa sasa, ni NAIC pekee ambacho kinafanya kazi.

Mikakati

--